Muwezeshaji wa mazungumzo ya maridhiano ya Burundi, Rais mstaafu wa Tanzania, Benjamin Mkapa.
Akiongea kwa niaba ya msuluhishi Mhe. Benjamin Mkapa, Davi Kapya, amesema mkutano umeenda vizuri na kuwa kazi kubwa inayo mkabili msuluhuishi ni kuipeleka ripoti maaluma ya maongezi hayo kwa maraisi ya nchi za jumuiya ya Afrika mashariki,
Kufuatia mkutano huo baadhi ya washiri akiwemo mwenyekiti wa muungano wa vyama vya siasi nchi Burundi Jean Didier Mutabazi wamemtaka msuluhishi kuhakikisha kuwa mazunguzo mengini yanafanyika nchini Burundi ili kutoa Fulsa kwa makundi mbalimbali kushiriki.
Hatua hiyo inaungwa mkono na msemaji wa chama CNDEDE, Gelase Ndabirabe ambaye amailezea kama hatua muhimu katika kufikia makubaliano ya amani nchini Burundi na kuongeza kuwa Azaki mbalimbali zitapata nafasi hiyo adhimu.
Mzunguzo hayo yamefanyika licha ya baadhi ya washiriki kueleza kutoridhishwa na mwenendo wake akiwemo Aloice Balichako, ambae ni mwenyekiti wa chama cha PARC De Part .
Mazungumzo ya amani ya siku nne yamemalizika bila ya kuelezwa tarehe kamili ya kukutana tena.