
“Mawakala wetu kwenye vituo 8 kati ya 13 katika kata ya Nyabubinza wamekamatwa na jeshi la polisi na kumekuwa na vitendo vingi tu vya kuharibu uchaguzi”, amesema Heche kwenye mahojiano ya moja kwa moja na eatv.tv kuhusu mwenendo wa uchaguzi katika kata hiyo.
Heche amemtaja Diwani Zakayo Chacha Wangwe kuwa ni miongoni mwa mawakala waliokamatwa wakati zoezi la uchaguzi likiendelea katika hatua ya upigaji Kura.
Aidha John Heche ameongeza kuwa hivi sasa katika vitu hivyo 8 ambavyo CHADEMA haina wawakilishi wamebaki mawakala wa vyama vya NCCR na CCM pekee.
Sheria ya Tume ya uchaguzi inakitaka chama kuwasilisha majina ya mawakala siku mbili kabla ya uchaguzi. Chama hutumia nafasi hiyo kuwaandaa mawakala pamoja na kuwaapisha kwajili ya kulinda maslahi ya chama ndani ya uchaguzi. Kwa maana hiyo basi kura katika vituo hivyo zitahesabiwa bila CHADEMA kuwa na wakala.