Wednesday , 10th Feb , 2016

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia, Ufundi na Mafunzo ya Ufundi nchini Tanzania Prof.Joyce Ndalichako amesema matumizi ya Mfumo wa Teknolojia ya Habari na mawasiliano TEHAMA

yamesaidia kupunguza kiwango cha udanganyifu kwa wanafunzi wa elimu ya juu nchini

Akizungumza leo jijini Dar es salaam katika uzinduzi wa Ripoti ya Maendeleo ya Bank ya Dunia, Prof.Ndalichako amesema kiwango cha ufanisi kimeongezeka katika mfumo mzima wa udahili kwa wanafunzi wanaojiunga na vyuo vya elimu ya juu pamoja na kurahisisha utunzaji wa kumbukumbu kwa wanafunzi wanaojiunga na vyuo hivyo kila mwaka na hivyo kuondokana na wanafunzi wengi kutumia matokeo ya mtu mmoja.

Prof Ndalichako ameongeza kuwa serikali ina mpango wa kuboresha mfumo wa ufundishaji wa TEHAMA katika shule za msingi na sekondari ili kurahisisha ufundishaji pamoja na kuwezesha wanafunzi kuwa na uelewa wa matumizi ya mtandao wakiwa katika shule za msingi.
Kwa upandev wake, mchumi Mwandamizi wa benki ya dunia Bi. Indhira Santos anasema Matumizi ya teknolojia ya TEHAMA yamesaidia katika nchi nyingi za Afrika ikiwa ni pamoja na Tanzania.

Akizungumzia fursa za ajira, mkurugenzi wa tume ya sayansi na teknolojia nchini Tanzania COSTECH, Dkt. Hassan Mshinda anasema changamoto kubwa iliyopo ni namna na kuendeleza ubunifu kwa vijana wengi wanaobuni nyenzo zinazotumika katika sekta mbalimbali nchini