Mashabiki sABA (7) wa timu ya soka ya simba ya jijini dar es salaam wamefariki dunia na wengine 13 kujeruhiwa, baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya costa kwenda mkoani shinyanga kushuhudia mechi baina ya timu hiyo na wakata miwa wa Kagera Sugar, kuacha njia na kupinduka katika eneo la kwa Makunganya, barabara kuu ya Morogoro - Dodoma.
Mashuhuda wa ajali hiyo waliokutwa eneo la tukio, wameiambia wamesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni utelezi uliosababishwa na mvua zilizokuwa zikiendelea kunyesha, uliomfanya dereva wa gari waliyokuwa wamepanda aina ya costa, yenye namba za usajili T304 CWN kushindwa kumudu na kuserereka kwa karibu kilometa 15, kabla ya kuvaa ukingo wa barabara na kupinduka na kusababisha vifo vya watu watano akiwemo Rehema Musa na Mohamed Kigolini maarufu kama ngumi jiwe, huku wengine wakijeruhiwa
Taarifa zaidi kutoka eneo la tukio zimebainisha kuwa majeruhi watatu kati ya 15 wa ajali hiyo hali zao zilikuwa ni mbaya, na wote wamekimbizwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro kwa matibabu,huku dereva wa gari hiyo akitokomea kusikojulikana.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP Leonard Paul amethibitisha habari hizi na kusema kuwa majeruhi wamebaki 13 na kufanya vifo kufikia saba hadi majira ya saa 2 usiku wa April 03.