Thursday , 13th Jul , 2017

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemuachia huru aliyekuwa Kamishna wa TRA, Tiagi Masamaki na wenzake watano waliokuwa wakishtakiwa na makosa ya kuhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara ya shilingi bilioni 12.7.

Washtakiwa hao wameachiwa baada ya upande wa mashtaka uliokuwa ukiongozwa na wakili wa serikali mwandamizi, Timon Vitalis kuiomba mahakama kufanya hivyo chini ya kifungu cha 91(1) ya makosa ya jinai (CPA) kwa kutoa taarifa kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya washtakiwa hao.

“Mheshimiwa Hakimu kesi hii leo imekuja kwa ajili ya kutajwa, hata hivyo tuna maombi...  DPP amewasilisha Nolle Prosque, hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya washtakiwa", amesema Wakili wa Serikali Timon Vitalis.

Hakimu Shahidi alikubaliana na ombi hilo na kuwaachia huru washtakiwa hao.