Waziri Simbachawene ameyasema hayo wakati akizungumza na East Africa Radio na kuongeza kuwa muelekeo wa jumla katika kutekeleza zoezi hilo la Rais linaonyesha baadhi ya wilaya wamemaliza kutengeneza madawati yaliyokua yanahitajika na kuondoa usumbufu huo wa madawati.
Amesema kwa baadhi ya mikoa ambayo haitakua imetekeleza zoezi hilo kikamilifu hadi kufikia Tarehe 30 Juni watawachukuliwa hatua za kiutendaji kwa mujibu wa maelekezo ya kazi yanavyoelekeza.
Kwa upande wao baadhi ya wakuu wa mikoa mbalimbali nchini akiwemo mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga amesema walikutana na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na ukosefu wa fedha kwa wakati,ukosefu wa mashine za kukausha mbao kwa haraka kwa ajili yakutengenezea madawati hayo.
Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amesema mkoa wake umekumbana na changamoto ya muda kuwa mdogo na ufinyu wa elimu kwa baadhi ya wananchi kwa ajili yakuchangia zoezi hilo.
Naye Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Steven Kebwe amesema kwa upande wa shule za Sekondari wamekamilisha lakini bado changamoto kidogo kwa shule za msingi.
Uhitaji wa madawati nchini ni takribani madawati Milioni tatu na laki tano.


