Saturday , 1st Oct , 2016

Watumishi wa manispaa ya Ubungo wakishirikiana na wananchi wa wilaya hiyo leo wamejitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la upandaji miti ikiwa ni kuunga mkono kampeni ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda

Katika halmashauri ya manispaa ya Ubungo zoezi hili lilitekelezwa katika maeneo ya Barabara za Nelson Mandela pamoja na Sam Nujoma ambapo vifaa mbalimbali viligawanywa miongoni mwa wananchi pamoja na miti ya kupandwa ambapo zoezi lilifanikiwa kwa kiasi kikubwa huku wanafunzi wa shule za sekondari za manispaa hiyo wakiongeza nguvu kwenye zoezi hilo

Kaimu afisa utumishi wa manispaa ya Ubungo Bw Joseph H Haule akielezea zoezi hilo alidai wameamua kuunga mkono agizo la mkuu wa mkoa kwani lina tija na litaleta manufaa si kwaajili yetu tu bali pia kwaajili ya vizazi vijavyo. Aliahidi kuwa yeye pamoja na manispaa yake ya Ubungo wataendelea na juhudi za kutunza mazingira ili kuufanya mkoa wa Dar es salaam kuwa sehemu safi na salama kwa kuishi

Zoezi la upandaji miti limefanyika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam ambapo makamu wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu alizindua zoezi hilo