Friday , 9th Sep , 2016

Kampuni moja nchini Kenya imeifungulia mashtaka Mamlaka ya Mapato nchini humo KRA, kwa madai mamlaka hiyo inashikilia shehena ya mchele iliyouagiza nchini humo licha ya kuwa umeshalipiwa kodi.

Jengo la Mamlaka ya Mapato nchini Kenya (KRA).

Kampuni hiyo ya Jamil Trading Ltd imesema kuwa haijatenda kosa lolote na kwamba imeshalipa kodi zote zilizodaiwa na Mamlaka ya Mapato Kenya.

Shitaka hilo kwa KRA limefunguliwa na kampuni ya uwakili ya Wameyo Onyango & Associates Advocates, ambayo imesema mteja wake anaendelea kupata hasara kwa uonevu wa KRA.