Monday , 28th Apr , 2014

Mke wa Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mama tunu Pinda ameziomba taasisi mbalimbali za afya kupunguza gharama za kutibu ugonjwa wa saratani.

Mke wa Waziri Mkuu, mama Tunu Pinda

Mke wa Waziri Mkuu wa Tanzania, Mama Tunu Pinda, ameziomba taasisi zinazojishughulusha na matibabu dhidi ya magonjwa ya saratani kuangalia uwezekano wa kupunguza gharama za matibabu hayo kwa wagonjwa wasio na uwezo.

Mama Pinda ametoa wito huo leo jijini Dar es Salaam mara baada ya umoja wa wake wa viongozi hapa nchini kutembelea hospital ya Aga Khan kwa lengo la kuangalia huduma za magonjwa ya saratani zinavyotolewa katika hospitali hiyo.

Amesema atatumia umoja huo kuhamasisha taasisi hizo kwa lengo la kuhakikisha kwamba hata wale wanaotoka maeneo ya vijijini na kukosa uwezo wa kutibu saratani wanasaidiwa kupata matibabu.