
Mh. Paul Makonda
Makonda ameweka wazi hilo leo ofisini kwake jijini Dar salaa na kusema anawahitaji vijana hao ili waunde mfumo utakaowawezesha wananchi kueleza kero yoyote aliyokutana nayo kwenye huduma za Umma.
''Nawaalika wote wenye utaalamu wa Teknolojia ya IT kufika ofisini kwangu Tarehe 01/11/2018 asubuhi kwaajili ya kuunda mfumo wa kuratibu uwajibikaji wa watendaji wa Umma ili kuhakikisha malalamiko ya wananchi yanashughulikiwa kwa haraka'', amesema.
Aidha Makonda amefafanua kuwa mfumo huo utakuwa ukipokea malalamiko ya watendaji wasiowajibika kuanzia ngazi ya Mitaa, Kata, Wilaya, Mkoa na viongozi Wakuu akiwemo Mkuu wa mkoa, Katibu tawala mkoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Makatibu tawala wilaya na wakuu wa idara watakuwa wakiona ni mtendaji gani asiewajibika kutatua kero za wananchi.
Mfumo utampa mwananchi uwezo wa kueleza malalamiko yake endapo amefika ofisi ya umma na watendaji kushindwa kushughulikia kero zake kwa uzembe.