.jpg?itok=4pvkgus3×tamp=1473705349)
Mhe. Samia ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza kwenye uzinduzi wa kongamano la nne la Kisayansi lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUHAS) ambapo amesema tafiti hizo zina lenga kupambana na ugonjwa wa Ukimwi, Kupunguza vifo vya mama na mototo, Malaria, na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Mhe. Samia ameeleza kuwa ili serikali iwe na wataalam wengi wanaojihusisha na tafiti za kisayansi hususani zile za masuala ya afya, ni vyema vyuo vya afya vinavyofanya tafiti hizo kushirikisha wanafunzi hasa wale wanaosoma shule za sekondari katika kazi zao za kitafiti kwani maendeleo ya nchi hayawezi kupatikana bila ya kuwepo na tafiti za kutosha za kisayansi.
Naye Makamu Mkuu wa Chuo hicho Ephata Kaaya amesema kuwa kongamano hilo litakalo dumu kwa muda wa siku mbili limewakutanisha wadau wa afya kutoka ndani na nje ya nchi kwa lengo la kubadilishana ujuzi na watafiti mbalimbali ambapo kauli mbiu ya mwaka huu kuwekeza katika afya na elimu ili kuleta maendeleo endelevu.