Friday , 27th Jan , 2017

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Njombe Bw. Christopher Ole Sendeka kuwachukulia hatua watumishi  Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa waliohusika na upotevu wa fedha za maendeleo.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipozuru mgodi wa Liganga wilayani Ludewa

 

Amesema zaidi ya sh. milioni 700 zilizopelekwa katika halmashauri kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo zikiwemo sh. milioni 300 za ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri hiyo.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Halmashauri alipokuwa katika ziara yake katika  Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe.

“Mkuu wa Mkoa watu wote waliohusika na upotevu huu watafutwe popote walipo na kuchukuliwa hatua na kisha nipewe taarifa ya hatua ulizochukua. Hatuwezi kuwavumilia watu hao ambao wanachora ramani kwa sh milioni 200  na sh. milioni 100 zingine hazijulkikani zilipo,“ alisema.

Pia Waziri Mkuu alimuagiza Mkuu huyo wa Mkoa  kufuatilia kiasi kingine cha sh milioni 400 zilizopelekwa wilayani hapo kwa ajili ya maendeleo ambazo nazo hazijulikani zilipo.

“Tafuta waliohusika popote walipo hata kama ni nje ya Njombe waje kutueleza ziliko fedha zetu,”

Awali akiwa njiani kuelekea Ludewa Mjini akitokea katika kata ya Mundindi Waziri Mkuu alisimamishwa na wananchi wa kijiji cha Mlangali ambao waliiomba Serikali iwasaidie kuzipatia ufumbuzi changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo ya maji.

Msikilize hapa na utazame video hapa