Akiongea na vyombo vya habari leo jijini Dar es salaam ,Jaji Chande amesema mahakama imeagiza majaji wafawidhi katika kila kanda kuangalia mahakimu zaidi ya 500 katika mahakama za wilaya na za mwanzo watoe maelezo kwa siku saba ili kila mmoja aeleze ni kwa nini hawajafikisha kiwango cha kumaliza kesi walizopangiwa kuzimaliza.
Jaji Chande amesema baada ya kujieleza watakaobainika kutokuwa na sababu ya kutosha watafunguliwa mashitaka ya kinidhamu za mahakama ili wachukuliwe hatua kutokana na kukiuka agizo la kuwataka kuwa na kiwango katika kuharakisha kumaliza mashauri.







