Tuesday , 22nd Dec , 2015

Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameungana na familia ya Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho katika Maziko ya Dada wa Rais Kikwete aitwaye Tausi Khalfan Kikwete aliyezikwa katika kijiji cha Msoga, Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya tano Mh. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete katika msiba wa dada yake Jakaya Kikwete

Tausi Khalfan Kikwete alifariki dunia tarehe 17 Desemba, 2015 huko Nchini India alikokwenda kwa ajili ya kupata matibabu.

Pamoja na Rais Magufuli viongozi wengine waliohudhuria maziko hayo ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Makamu wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Mawaziri na viongozi wengine wakuu wa Serikali.

Ibada ya Maziko imeongozwa na Mufti wa Tanzania Alhaji Abubakar Zuberi.