Monday , 31st Aug , 2015

Mgombea Urais kupitia chama cha Mapinduzi CCM, Dkt. John Pombe Magufuli amemaliza ziara yake katika mkoa wa Njombe na kuwaomba Watanzania kumchagua kwa kuwa ana mpango wa kuijenga Tanzania mpya ndani ya Chama hicho.

Mgombea urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli mkoani Njombe jana.

Dkt. Magufuli amesema hayo wakati akimaliza Ziara yake katika Kijiji cha Mlangali Wilayani Ludewa na kuongeza kuwa serikali nne zilifanya makubwa katika kuboresha mazingira ya Maendeleo hivyo awamu yake itakua ni kukamilisha mabadiliko.

Aidha ameongeza kuwa kutokana na Mafaniko ya Serikali zilizopita, awamu ya Tano itakua ni ya Maendeleo ya Barabara, Umeme, Viwanda, Elimu, Maji, Afya, Ajira na kuboresha mazingira ya Wafanyakazi na Wakulima.

Katika mikutano yake ya jana Wilayani humo Dk. Magufuli ambae leo anaanza rasmi Kampeni mkoani Ruvuma amesema atashughulikia ipasavyo matatizo yote ya uhaba wa maji na Umeme.