Mkuu wa mkoa wa Njombe Dkt.Rehema Nchimbi
Mkuu wa mkoa wa Njombe Dkt.Rehema Nchimbi akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa zuio hilo linawahusu wafanyabiashara wanaotumia magari yenye uzito unaozidi tani 30 ambapo ndani ya miezi hiyo watatakiwa kupata vibali vya kupitisha uzito huo na baada ya hapo hakuta kuwa na vibali vya kupitisha uzito huo.
Amesema kuwa wafanyabishara hao watapitisha mizingo yenye uzito wa kuanzia tani 30 kushuka chini kwa kukata vibali ofisi za wakala wa barabara Tanzania mkoa wa Njombe Tanroads kwa kulipia dola 20 na baada ya miezi hiyo miwili hakutaruhusiwa uzito unaozidi tani 10.
Amezitaja barabara zinazo husika na zuio hilo baada ya miezi miwili kuwa ni pamoja na barabara ya Kibena mpaka Lupembe kuunganisha na mkoa wa Morogoro, barabara ya Rambazani Njombe mjini, mpaka wilayani Makete na barabara ya Itoni njombe mjini mpaka wilayani Ludewa ambazo zimeingizwa katika mpango wa kukarabatiwa kwa kiwango cha lami.
Walengwa wa agizo hili ambao kwa sehemu kubwa ni wasafirishaji wa mazao kutoka sehemu mbalimbali za mkoa wakiwemo madalali wamepokea kwa hisia tofauti agizo kwa kuhofia mtikisiko wa uchumi.
Pamoja mawazo mazuri ya serikali wadau wa usafirishaji wakiwemo madalali na wakulima hawajashirikishwa kutoa maoni yao na wangetakiwa kujiandaa kuepuka madhara ya kudorola kwa uchumi