Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Mohamed Mpinga
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salam Kamanda Mohamed Mpinga amesema mfumo huo ambao ni utekelezaji wa kanuni mpya za usalama barabarani utaanza kutumika kesho kwa jiji la Dar es salaam kwa majaribio na baadaye nchi nzima.
Kamanda Mpinga ameongeza kuwa mfumo huo utawezesha madereva waliokamatwa na makosa mbalimbali wata lipa kwa njia ya simu au kadi ya benki yoyote.
Aidha kamanda Mpinga amesema kuwa pia kutakuwa na kamera maalum ambazo zitawekwa barabarani zenye uwezo Wa kutambuwa madereva walioshindwa kulipa faini, makosa ya gari, uhalali Wa leseni, mwendo kasi, kadi na vibali vya gari husika pamoja na kujua kama Dereva amelipa faini au bado.
Afande Mpinga ameongeza kuwa mashine hizi za kielectroniki zitaweka alama za nundu katika leseni zenye makosa na yakifika makosa 15 leseni ya dereva husika itafungiwa kwa miezi 6.