Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Arusha Harson Mwakyoma amesema wamejipanga kikamilifu kukabiliana na watu wanaotishia kuwashambulia madereva na abiria kwa kuweka askari maeneo yote makorofi na pia kuyasindikiza mabasi .
Aidha kamanda Mwakyoma pia amewaasa madereva kuacha kuthamini kazi zao na kuepuka kutumiwa na baadhi ya watu wenye malengo ya kuwagombanisha na serikali na pia na wamiliki wa mabasi.
Wakizungumzia hali hiyo baadhi ya wadau wameendelea kuitaka serikali kuanza kuangalia upya namna ya kuweka utaratibu endelevu wa kuwawezesha madevera kufanya kazi zao kwa salama na amani bila kuonewa na kuingiliwa na watu ama idara nyingine.