
Lwakatare ameyabainisha hayo alipokuwa akifanya mahojiano na kituo cha EATV, kuhusiana na vifaa vyake alivyopeleka kwa ajili ya kusaidia wajawazito katika vituo vya afya jimboni kwake kukataliwa kwa kile kilichodaiwa kuwa ni hadi mganga mkuu wa wilaya ajiridhishe kama vinahitajika.
''Kina mama katika jimbo langu na maeneo mengine wanateseka kupeleka vifaa vya kujifungulia kama glovs,mabeseni,wembe na dawa ya kuongeza uchungu nikanunua vifaa hivyo katika duka la MK phamacy Bukoba mjini cha kushangaza ni kwamba mganga mkuu akakataa kutoa ushirikiano wakati niliandika barua ya kumtaarifu mganga mkuu wa mkoa kuhusu ziara yangu hiyo kwa vituo hivyo'' Amesisitiza Lwakatare.
Lwakatare ameongeza kuwa muda waliokubaliana kupeleka vifaa hivyo mganga mkuu wa manispaa ya Bukoba hakuonekana kwa masaa mawili na alipowasili ilibainika kuwa ametoka kwenye kikao na viongozi wa CCM wa wilaya ndipo akagoma kutoa ushirikiano na swala hilo lipo kisiasa japo kwa sasa walitakiwa viongozi wote waungane kufanya maendeleo.
Aidha Lwakatare ameitaka serikali kuwapa semina elekezi watendaji wao na kuacha kutumika kisiasa na badala yake wajikite katika kutatua matatizo ya wananchi.
Hata hivyo amebainisha kwamba amefanya mkutano wa kihistoria na wanabukoba waishio ndani na nje ya nchi kuhusiana na namna ya kusaidia kutatua matatizo ya wananchi wake.
Wakati huohuo katibu mkuu wizara ya afya , maendeleo ya jamii, jinsia na watoto Dkt Mpoki Ulisubisya amesema misaada inayotolewa na watu mbalimbali kwa ajili ya kusaidia jamii lazima ikidhi vigezo vya kiafya na kisheria.