Mgombea Urais aliesimamishwa na Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA, kupitia CHADEMA, Mh. Edward Lowassa.
Akiongea na maelfu ya wananchi waliojitokeza katika viwanja vya Tanganyika Packers jijini Dar es Salaam, Lowassa amesema kuwa vipaumbele hivyo ni vitu ambavyo ana uhakika navyo na atavimudu kuvimaliza ndani ya siku hizo.
Lowassa ameongeza kuwa pamoja na vipaumbele hivyo ikiwemo elimu bure ambayo ndiyo itakuwa mkombozi kwa taifa pia ataboresha idara mbalimbali ikiwemo kufuta kodi kwa wafanyabiashara, kutatua tatizo la maji, Foleni Dar es Salaam na mengineyo.
Mhe. Edward Ngoyai Lowasa amesema akichaguliwa kuwa Rais wa Tanzania atahakikisha anasimamia utoaji wa elimu kwa ufanisi mkubwa ikiwa ni pamoja na kufuta ada zote kutoka chekechea hadi chuo kikuu.
Awali akizungumza katika mkutano huo, mwenyekiti wa Chadema Mhe.Freeman Alkael Mbowe amesema wanaomba ridhaa ya kuongoza serikali ili kuwashughulikie kero nyingi zinazowakabili wananchi.