
Kufufuka kwa Yesu ni ishara ya ushindi dhidi ya dhambi za asili kwa wanadamu, baada ya Yesu Kristo kuchukua umaskini wa mwili na kiroho kwa kukubali kusulubiwa na kufa msalabani ili wanadamu wapate msamaha wa dhambi.
Akizungumzia siku ya leo, kiongozi wa huduma ya Mikocheni B Assemblies of God, mchungaji Dkt Getrude Lwakatare amesema siku ya leo ni ya furaha kwa jumuiya ya wakristo na kwamba kuna haja ya wakristo nchini kuiadhimisha siku hii kwa kutenda mema kama Yesu mwenyewe alivyoamua kujitoa na kufa msalabani kwa ajili ya wanadamu.