Afisa uhusiano wa PSI kanda ya njanda za juu kusini, Sanday Beebwa.
Akizungumza na East Africa Radio katika viwanja vya Sabasaba mkoani njombe, afisa uhusiano wa PSI kanda ya njanda za juu kusini, Sanday Beebwa amesema kuwa katika vitu vinavyo ongeza kasi ya maambukizi mkoani humio na Tanzania kwa ujumla ni pamoja na tamaduni na mila.
Beebwa amesema sasa wameanza kushierikiana na viongozi mbalimbali wa dini na viongozi wa kisiasa ambao wanawasihi kutoa elimu kwa wanachi wanapo kutana nao popote pale katika mikutani yao.
Aidha Beebwa ameongeza kuwa katika mikoa mitano ya juu Mikoa ya Nyanda ndio inaongoza huku mkoa wa njombe ukiwa ndio mkoa pekee Tanzania wenye tarakimu mbili za Kitakwimu katika Maambukizi
Maadhimisho haya ambayo kilele chake ni leo ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal.