Katiba Inayopendekezwa.
Wakizungumza katika mkutano wa hadhara ulioitishwa kituo cha sheria na haki za binadamu kwa kushirikiana na tume ya taifa ya uchaguzi wakazi hao wamesema mapendekezo mengi waliyowasilisha katika rasimu ya kwanza ya katiba kwa mwenyekiti wa tume hiyo jaji Joseph Sinde Warioba yamepunguzwa hivyo ni lazima tume ijipange upya ili kuleta Demokrasia ya kweli nchini.
Kwa upande wake mwenyekiti wa wazee wa wilaya ya Muheza akielezea suala ya uhesabuji wa kura mara baada ya ya siku ya upigaji kura kufika, ameiomba tume ya taifa kufanya mabadiliko kwa waratibu wa uchaguzi ambao ni wakurugenzi wa halmashauri katika mchakato huo na badala yake watafutwe watu wa makundi tofauti yenye heshma kwa sababu watakosa imani ya kupata takwimu sahihi za waliopiga kura ya hapana na ndio.
Kufuatia hatua hiyo mratibu wa kampeni ya utoaji elimu kwa wananchi kuhusu Katiba Pendekezwa wa kituo cha sheria na haki za binadamu mkoa wa Tanga Bwana Stanley Gumbo amewataka wananchi kuzingatia elimu ya katiba zoezi hilo la kitaifa lengo lake ni kutaka wananchi wakubali kwa ridhaa yao ili kupata Katiba mpya.