Thursday , 17th Mar , 2016

Waziri wa afya, maendeleo ya jamii,jinsia wazee na watoto wa Tanzania Ummy Mwalimu amesema kuwa tatizo la ukeketaji nchini bado linachangamoto nyingi za kulidhibiti kutokana na watu wengi kuendekeza mila na desturi na kufanya vitendo hivyo kwa siri.

Waziri wa afya, maendeleo ya jamii,jinsia wazee na watoto wa Tanzania Ummy Mwalimu

Akiongea katika Mkutano wa 60 wa kamisheni ya hali ya wanawake duniani CSW60,Jijini New York, Waziri Ummy amesema kati ya changamoto hizo ni pamoja na kuwepo kwa kisingizio cha mila hivyo kuwanyia watoto ukeketaji kwa kificho na wakati mwingine imefikia hatua hadi kuwakeketa wakiwa wachanga.

Waziri Ummy amesema kuwa ili kabiliana na suala na kulitokomeza kabisa serikali imeweka mipango madhubuti katika sehemu ambazo zimekithiri kwa vitendo hivyo ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa kwa sheria ya makosa ya jinai kwa wanaofanya vitendo vya ukeketaji.

Aidha Mhe. Ummy ameongeza kuwa sheria pekee haitoshi kumaliza tatizo hilo hivyo wamenzisha mfumo maalumu ya kuwajengea uelewa wananchi juu ya ufahamu wa madhara wanayoyapata watoto baada ya kufanyiwa tendo hilo.