Thursday , 4th Jul , 2019

Mahakama Hakimu Kazi Kisutu leo Julai 4 imemuachia huru msanii wa filamu nchini, aliyewahi kuwa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu lakini baada ya muda mfupi, Askari Magereza wakamkamata tena.

Wema Sepetu

Wema ambaye anakabiliwa na shitaka moja la kuchapisha video na picha za faragha na kuzisambaza katika mtandao wa Instagram kinyume cha sheria.

Ikumbukwe kuwa June 24, mahakama hiyo ilimuonya kutokiuka masharti ya dhamana la sivyo mahakama itamfutia dhamana yake.

Hakimu Mkazi Mkuu, Maira Kasonde alimuachia huru mshtakiwa huyo kwa sheria ya kifungu cha 225(5), cha mwenendo wa mashtaka ya makosa ya jinai.

Katika kesi ya msingi Wema anadaiwa kutenda kosa hilo Oktoba 15, 2018,  katika maeneo ya jiji la Dar Es Salaam,  alirekodi video ya ngono na kuisambaza katika ukurasa wake wa kijamii wa Instagram.