Thursday , 20th Mar , 2014

Serikali ya Tanzania imetumia shilingi bilioni 7.9 kununua kivuko chenye uwezo wa kubeba abiria mia tatu kati ya Dar es Salaam na Bagamoyo mkoani Pwani ili kupunguza msongamano wa magari kati kati ya Jiji la Dar es Salaam.

Hayo yameeleza leo jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi nchini, Bw. MartinNtemo, wakati akizungumzia namna wizara hiyo inavyosimamia ujenzi wa vivuko, barabara na makazi ya watumishi katika mikoa mbalimbali nchini.

Bw. Ntemo ameongeza kuwa ujenzi wa kivuko cha Bagamoyo unaendelea huku kivuko kikitarajiwa kuwasili nchini mwezi Mei mwaka huu,wakati pia serikali ikiendelea na ukarabati wa vivuko vya MV Geita na MV Kome 1 vya Jijini Mwanza.