Friday , 10th Oct , 2014

Jeshi la polisi mkoa wa Arusha limefakiwa kumuua mtu mmoja anayedaiwa kuwa ni kinara wa kundi linalojihusisha na  uporaji pamoja  na mauaji ya wanawake unaoendelea katika jiji la Arusha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, ACP Liberatus Sabas

Jeshi la polisi mkoa wa Arusha limefakiwa kumuua mtu mmoja anayedaiwa kuwa ni kinara wa kundi linalojihusisha na  uporaji pamoja  na mauaji ya wanawake unaoendelea katika jiji la Arusha baada ya majibizano ya risasi kati ya askari wa jeshi hilo na jambazi huyo yaliyotokea katika eneo la moivo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabasi amesema tukio hilo limetokea majira ya saa Nane usiku baada ya jeshi hilo kufanya uchunguzi na kugundua mahali anapoishi Ramadhani Abdallah Jumanne na kutaka kumkamata na yeye kuanza kurushiana risasi na askari lakini walifanikiwa kupiga risasi na alifariki njiani akipelekwa hospitali.

Kamanda Sabasi amesema mtu huyo anahusishwa na matukio ya mauaji yakiwemo ya Shamim Rashidi na mtoto wa miaka mitatu Christina Nickson yalitokea hivi karibuni lakini pia amekutwa na pikipiki yenye vibao tofauti vya namba za usajili na  bastora aina ya Rock 19, yenye magazini Nne na kifaa cha kuona mbali na kurenga shabaha  katika bastola,  pamoja na Radio ya upepo iliyokuwa inamilikiwa na mahakama ya kimataifa ya kimbali ICTR iliyokuwa imeibwa.

Wakiongea na EATV katika kituo cha polisi mkoa wa Arusha watu wanaodai kuporwa na kunusurika kuuawa na jambazi huyo wamekiri kumtambua mtu huyo na kulitaka jeshi la polisi liongeze jitihada za kugombana na waharifu pamoja na wananchi kujenga tabia ya kushirikiana  panapo kuwa na matukio ya aina hiyo.