Wednesday , 1st Jul , 2015

Wananchi wa kijiji cha Rwangu wanatarajia kupanda hekta 51 za chai ambayo baada ya kukoamaa kutakujengwa kiwanda kikubwa Tanzania cha chai ambacho kinaundwa nchini Kenya na kurahisisha uuzaji zao hilo likiwa limesindikwa.

Wakulima wakiwa shambani wakati wa kuvuna chai.

Wakisoma taarifa ya utekelezeji wa upandaji wa mashamba ya chai Mkoani Njombe wananchi wa kijiji cha Rwangu halmashauri ya mji Njombe wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru wamesema kuwa wamefanikiwa kupanda hecta 15 za chai na hekta 36 wanatarajia kuanza kupanda msimu ujao.

Akisoma kwa niaba ya wakulima hao mwenyekiti wa kikundi hicho cha Ruangu Tea Block Brasius Luiva alisema kuwa kilimo hicho cha chai kitakuwa mkombozi wa wakulima wa kijiji hichi kwa kuwa chai yao itaanza kwa kuuzwa 250 kwa kilo ikifika kiwandani na kuwa kunatarajiwa kujengwa kiwanda kikubwa kulivko vyote Tanzania.

Aidha kwa upande wake kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Juma Hatibu Chumu amesema kuwa Tanzania kwa uchumi inategemea kilimo na kuwataka wakulima hao kulima kisasa na kunufaika na kilimo hicho.