Thursday , 19th Jun , 2014

Raisi Jakaya Kikwete ameendelea kutekeleza ahadi zake ambapo leo umoja wa waendesha bodaboda jijini Arusha umekabidhiwa pikipiki kumi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete.

Akikabidhi pikipiki hizo kwa niaba ya rais kikwete, mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo amewataka waendesha boda boda kuendelea kujiunga na vikundi ili wawe na sauti moja itakayo wasaidia kufikia malengo yao.

Mwenyekiti wa waendesha bodaboda Godlight Rugemalila ameiomba jamii kuiangalia kazi ya bodaboda kama kazi zingine.

Wakipokea bodaboda hizo Jamal Juma na Steven Laizer wamesema pikipiki hizo zitawasaidia kutoka katika hali ya kuajiriwa na kuweza kujiajiri.

Hii ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa Rais Jakaya Kikwete alipokua akizindua jiji la Arisha tarehe 1 Mwezi wa 11 Mwaka 2014.