Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangalla
Naibu Waziri huyo ametoa agizo hilo wakati wa uzinduzi wa utekelezaji wa kuimarisha huduma ya afya ya mama, wajawazito, watoto wachanga na watoto walio chini ya umri wa miaka mitano wilayani Geita.
Dkt. Kigwangalla amesema kuwa muda huo ukipita bila agizo hilo kutekelezwa atawawajibisha viongozi hao kwani wameteuliwa kwa ajili ya kuisaidia serikali katika kuboresha sekta mbalimbali ikiwemo ya afya pamoja na maendeleo ya jamii kwa ujumla.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika lisilokuwa la kiserikali, AMREF, Dkt. Frolence Teme amesema wameamua kufanya mradi katika mkoa wa Geita kwani ni moja kati ya mikoa yenye changamoto ya wajawazito wengi kujifungulia majumbani.