Wednesday , 5th Aug , 2015

Hatimaye wanachama wa CCM katika majimbo mawili ya wilayani Tarime Mkoani Mara wamepiga kura za maoni baada ya kuharishwa kwa siku mbili mfululizo huku waziri wa kazi na ajira mh gaudentia kabaka na Mh nyambari Nyangwine wakiangushwa.

Waziri wa Kazi na Ajira ambae pia alikua anagombania kupitishwa kugombea Jimbo la Tarime Mjini Gaudensia Kabaka akizungumza katika moja ya mikutano na Umoja wa Madereva

Akitangaza matokeo ya majimbo ya Tarime Mjini na Tarime Vijijini chini ya ulinzi wa askari polisi mkurugenzi wa uchaguzi huo wa CCM, katika majimbo hayo bw Mathias Lugola,amesema katika jimbo la Tarime mjini bw Michael Kembaki ameshinda nafasi hiyo kwa kupata kura 3,908 dhidi ya wagombea wengine watano akiwemo Mh. Kabaka.

Jimbo la Tarime Vijijini bw, bw Mathias Lugola akitangazwa kuwa mshindi kwa kupata kura 15,928 dhidi ya wagombea wengine saba wakiongozwa mbunge anayemaliza muda wake Mh Nyambari Nyangwine.

Hata hivyo akizungumza na vyombo vya habari baada ya zoezi hilo la kupiga kura na matokeo hayo kutangazwa, mbunge anayemaliza muda wake ambaye alikuwa mgombea wa jimbo la Tarime vijijini mh Nyambari Nyangwine, amedai kuwa mchakato mzima wa kampeni hadi zoezi la upigaji wa kura lilikiuka taratibu zote za chama hicho.

Kwa upande wao baadhi ya washindi katika majimbo hayo mawili wilayani Tarime, wamewashukuru wapiga kura ambao wamewahamini na kuwapa ushindi huo mkubwa.