
Wabunge wateule wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamemchagua Mh .Jobu Ndugai kuwa spika wa bunge hilo baada ya kupiga kura ya kumchagua spika wa bunge hilo nafasi iliyokuwa inawaniwa na wagombea wanane kutoka vyama mbalimbali vya siasa nchini.
Akitoa matokeo hayo mwenyekiti Mwenyekiti wa Uchaguzi huo, Mhe. Andrew Chenge amesema spika Ndugai amechaguliwa na kushinda kwa jumla kura 254 ya idadi ya wabunge ambayo ni sawa na asilimia 70 ya kura zote.
Baada ya kupigiwa kura na kutajwa kuwa spika wa bunge la 11 aliapishwa mbele ya katibu wa bunge na kutoka kwaajili ya kubadili mavazi na kuingia kwaajili ya kufungua kikao cha kuapisha wabunge.
Hata hivyo baada ya kufungua kikao cha kwanza cha bunge hilo Mh Ndugai ameahidi kusimamia sheria na demokrasia katika vikao bungeni na kuhakikisha hoja zinazotolewa kwaajili ya maendeleo ya wananchi zinafanyiwa kazi.