Friday , 2nd Oct , 2015

Maofisa Wawili wa Jeshi la Wananchi Tanzania(JWTZ) wapotea baada ya ndege ya kufundishia waliyokuwa wanatumia kudaiwa kuangukia kwenye bahari ya hindi eneo la Kawe Jijini Dar es Salaam na kuzama jana.

Kanali Ngemela Lubinga (katikati).

Msemaji wa Jeshi la Wananchi JWTZ, Kanali Ngemela Lubinga amesema jana kuwa jeshi hilo linaendelea kuwatafuta wanajeshi hao kwa ushirkiano wa vyombo vya majini na anga.

Kanali Lubinga amearifu kuwa ndege hiyo ya kufundishia marubani wa kijeshi ilianguka saa 3 Asubuhi ikiwa na maofisa wawili ambao ni mwalimu na mwanafunzi wake mmoja.

Katika tukio jingine wanajeshi sita wa jeshi la kujenga taifa JKT, kambi ya Bulumbola wamefariki na wengine 21 kujeruhiwa baada ya gari waliyokuwa wanasafiria kupinduka jana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Ferdinand Mtui amesema ajali hiyo ilitokea jana saa kumi jioni katika mlipa pasua uliopo kati ya wilaya ya Uvinza na Kigoma Mjini.