Tuesday , 6th Oct , 2015

Rais wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wameahidi kudumisha ushiriakiano baina ya nchi hizo mbili hata wakati ambao Rais Kikwete atakapotoka Madarakani.

Rais wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta

Wakizungumza katika uzinduzi wa Mradio wa Barabara unayounganisha Kenya na Uganda kupita mpaka wa Holili mpaka tatia Taveta jana marais hao wamesema umoja wa nchi hizo mbili utakua chachu ya kuleta maendeleo ukanda wa afrika mashariki.

Aidha marais hao wamesema kuwa uhusiano wa wananchi wa Tanzania na Kenya unatakiwa kuunganishwa na serikali zote mbili ikiwa ni pamoja na serikali kuwaunganisha wananchi hao kupita miundombinu ikiwemo barabara.

Katika hatua nyingine Kikwete amesema kuwa mradi wa barabara ya Holili mpaka Taveta utakapokamilika utarahisha muda wa wafanyabiashara kusafirisha bidhaa zao katika nchi za Afrika Mashariki.

Rais Kikwete amesema kuwa wafanyabiashara walikuwa wanatumia muda mwingi kukaa njiani kwa muda mrefu kuelekea nchi za Afrika Mashariki.

Aidha wakazi wa nchini Kenya wamesema kuwa ufunguzi wa barabara hiyo pamoja na ziara ya Rais Kikwete nchini Kenya itafungua mipaka zaidi ya biashara na kukuza uhusiano wa biashara baina ya nchi hizo mbili.