Thursday , 8th Oct , 2015

Rais Kikwete amesema kuwa kuna haja ya kurekebisha baadhi ya sheria za Ujenzi wa nyumba na Manunuzi ili kuweza kuwa na Mji wa kisasa na kupunguza misongamano katika makazi ya watu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.

Rais Kikwete amesema hayo jana Jijini Dar es Salaam wakati wa akiweka jiwe la msingi kwenye mradi wa nyumba wa shirika la Nyumba (NHC) lijulikanalo kama morocco Square.

Rais Kikwete amesema kuwa miradi ya aina hiyo itasaidia lakini zinahitajika sheria za kuhakikisha miradi ya ujenzi wa kisasa imefanikiwa na kuweza kuwasaidia wananchi wa hali zote kuweza kuyamudu.

Rais Kikwete ameongeza kuwa Dar es Salaam ni eneo dogo lenye msongamano mkubwa wa watu ambao wengi wao hawana makazi bora ya kuishi hivyo shirika hilo linapswa kuboresha makazi hayo kwa kujenga nyumba za bei rahisi.