Monday , 9th May , 2016

Watanzania wakiwemo wabunge wa bunge la Tanzania, wameombwa kuwekeza katika viwanda vidogo ili kuepusha bidhaa zinazowezwa kutengenezwa nchini zisiagizwe kutoka nje ya nchi, na kusaidia kuongeza pato la taifa.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage.

Akiongea Bungeni leo Mjini Dodoma katika kipindi cha Maswali na Majibu, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage, amesema kuwa kuna bidhaa ambazo zinahitaji mitaji midogo kuwekeza lakini watanzania wengi hawajazipa kipaumbele katika uwekezaji.

Mhe. Mwijage, amesema kuwa gharama za kuagiza mtambo wa kutengenezea bidhaa kama toothpick mtaji wake ni Mtanzania yoyote mwekezaji anaweza kuagiza hivyo hata bunge likipiga marufuki uingizwaji wa bidhaa hiyo kama kuna mtanzania atajitokeza kuwekeza italeta faida.

Katika hatua nyingine Waziri huyo wa viwanda amemtaka Mkurugenzi wa Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo (SIDO) kufanya ziara Mkoani Tanga kuangalia kiwanda cha juisi kilichosimamisha uzalishaji ili kutatua tatizo hilo kwa haraka.

Sauti ya Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage,