Wednesday , 17th Feb , 2016

Serikali imesema hairidhishwi hata kidogo na utendaji kazi unaofanywa na wakala wa serikali wa umeme na ufundi Temesa katika uendeshaji wa shughuli za vivuko nchini pamoja na ukusanyaji wa mapato.

Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa

Akizungumza na wafanyakazi wa wizara ya ujenzi,uchukuzi na mawasiliano mkoani mara, waziri wa wizara hiyo mhe. Prof Makame Mbarawa,amesema katik siku za hivi karibuni serikali italazimika kuchukua uamuzi mgumu hasa kwa kufanya mabadiliko ya watendaji wote wa wakala huyo ili kuongeza uwajibikaji.

Katika mkutano huo waziri huyo amesema serikali pia imepanga kutumia dola milioni 3o kwa ajili ya matengenezo na ukarabati mkubwa wa uwanja wa ndege wa Musoma mkoani Mara.

Amesema hatua hiyo imelenga kuwaondolea kero wanayoipata wananchi wa mkoa wa Mara wakiwemo watalii wanaofika mkoani humo kabla kutembelea hifadhi ya taifa ya Serengeti ikiwa ni njia moja wapo ya kumuenzi baba wa taifa hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Kuhusu kampuni ya simu nchini TTCL, waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Mh. ameitaka kampuni hiyo kuacha ukilitimba kwa kuitegemea serikali katika kufanya biashara hiyo na kwamba wanapaswa kuongeza wateja na katika kukuza ukusanyaji wa pato la taifa.