Tuesday , 1st Nov , 2016

Viongozi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, wamesema wamekuwa na mikakati mbalimbli ya kimaendeleo hususani kwa upande wa utunzaji wa mazingira pamoja na miundombinu ili jiji hilo liwe la mfano Afrika Mashariki.

Muonekano wa Jiji la Arusha

Athumani Kihamia ni mkurugenzi wa jiji la Arusha amesema mikakati yao mingine ni pamoja na kuongeza mapato kwa ajili ya maendeleo ya halmashauri ya jiji ili liwe la mfano kwa nchi za Afrika Mashariki kwa kuvutia watalii kwa maliasili ilizonazo.

Lakini kwa upande wake Naibu Meya wa Jiji hilo, Viola Lazaro amesema kuwa licha ya maendeleo ya jiji hilo lakini bado uongozi wa halmashauri unakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa ardhi ambapo wanalazimika kununua ardhi kwa baadhi ya maeneo kutokana na maeneo ya awali kuuzwa kinyemela.

Aidha kwa upande wao baadhi ya wakazi wa jiji hilo wamekuwa na maoni tofauti kuhusu maendeleo ya jiji hilo huku wengine wakisema kasi ya maendeleo inaridhisha lakini bado kuna changamoto ya ufufuaji wa viwanda vilivyokufa vilivyopo jijini humo.

Mkurugenzi wa jiji la Arusha Athumani Kihamia.