Friday , 24th Jun , 2016

Jeshi la Polisi kesho litazindua mpango wa maboresho ya jeshi la polisi ambao una lengo la kuleta mageuzi ya utendaji kazi katika kuwahudumia wananchi kwa kuzingatia weledi, sheria pamoja na haki za binadamu.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Ernest Mangu

Akizungumza na East Africa Radio leo, Mkuu wa Mpango huo, Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi, Goodluck Mungi, amesema kuwa jeshi la polisi limekuwa na taswira mbaya kwa wananchi ikiwemo kuwaonea wananchi hivyo kupitia mpango huo wataweza kutatua changamoto hizo na kurudisha heshima ya jeshi hilo.

Kamanda Goodluck Mungi amesema moja kati ya maboresho ya jeshi hilo ni pamoja na kuwa na kituo cha upokeaji simu na kufikisha taarifa kwa haraka ili kuweza kutatua tatizo pamoja na kusambaza vituo vya kuhamishika katika maeneo mengi korofi.

Naibu Kamishna huyo amesema mpango huo utaanzia kwa Wilaya ya Kinondoni kwanza, lakini wakiwa na lengo la kusambaa nchi nzima na kusema mpaka sasa wataweka vituo vya kuhamishika (Mobile Station) katika maeneo korofi 13 yaliyogundulika katika wilaya hiyo.

Amesema mpaka sasa kwa wilaya ya Kinondoni wanahitaji askari wa ziada 988, magari 55 yaliyofungwa mfumo wa GPRS na pikipiki 123 kwa Kinondoni pekee pamoja na vifaa vingine vya kusimamia mpango huo uweze kufanyika kwa ufanisi.

Sauti ya Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi, Goodlack Mungi,