Rais wa Chama cha Madaktari wa Afya ya Kinywa na Meno Tanzania (TDA), Dk. Lorna Carneiro
Mratibu wa maadhimisho ya siku ya afya ya kinywa na meno mkoa wa Mbeya, Dkt. Fredrick Meena, ametoa hamasa hiyo kwenye kilele cha maadhimisho hayo ambacho kwa mkoani Mbeya kimefanyika Jumamosi hii ikiwa ni siku moja kabla ya kufanyika kwa maadhimisho hayo kitaifa mkoani Morogoro.
Dkt. Meena amesema matatizo ya meno yameendelea kuikumba jamii kutokana na watu wengi kutozingatia misingi ya usafi wa kinywa na meno ambapo baadhi huamini kutumia na dawa na mswaki inatosha kwa usafi pasipo kujali ubora wa zana hizo.
Kwa upande wake kaimu mkuu wa chuo cha afya ya kinywa na meno cha Mbeya Ibrahim Kasambala, amesema katika kuelekea kilele cha maadhimisho hayo shughuli mbalimbali zimefanywa na wataalamu na wanafunzi wa chuo chake ikiwemo kutoa elimu na tiba sambamba na kuwabaini wanafunzi walio na matatizo ya meno katika kituo cha walemavu Tazara, mahabusu ya watoto Mwanjelwa, kituo cha yatima cha Nuru na shule za sekondari za Iganzo na Wigamba.
Naye mkuu wa idara ya kinywa na meno katika hospitari ya rufaa kanda ya Mbeya Dkt. Omary Khamis ameshauri huduma ya elimu ya afya ya meno kutosubiri wakati wa maadhimisho pekee huku akisisitiza kuwa ukiwa na afya njema ya kinywa itapelekea kuwa na afya njema ya mwili mzima.