Friday , 6th May , 2016

Serikali ya Mkoa wa Iringa imesema imeamua kuanzisha Harambee kwa kila Mkazi na Mwenyeji wa Mkoa huo anaeishi ndani au nje ya mkoa katika kuchangia kumaliza tatizo la madawati na changamoto za elimu mkoani humo.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi Amina Masenza akipongezana na mkuu wa Wilaya ya Iringa Bw Richard Kasesela

Serikali ya Mkoa wa Iringa imesema imeamua kuanzisha Harambee kwa kila Mkazi na Mwenyeji wa Mkoa huo anaeishi ndani au nje ya mkoa katika kuchangia kumaliza tatizo la uhaba wa madawati na changamoto zingine za elimu.

Akiongea leo Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza amesema licha ya Mkoa wake kuwa na rasimali nyingi za miti lakini wanakabiliwa na tatizo la rasimali fedha katika utengenezaji wa madawati hayo ambapo wametakiwa na rais hadi kufikia mwezi Juni wawe wamemaliza tatizo hilo.

Bi. Masenza amesema kuwa licha ya kutaka kulimaliza tatizo haraka lakini pia ni muhimu sana kwa mwanafunzi kukaa juu ya madawati pamoja na mazingira mazuri ya kusomea ili kukuza ufaulu wa wanafunzi.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela, amesema kuwa kuna watu wahujumu rasilimali misitu kwa kigezo cha kutengeneza madawati na kusema jambo hilo halikubaliki na serikali itachukua hatua kwa atakaebainika kufanya hivyo.