Wednesday , 3rd Dec , 2014

Shirika la kazi la umoja wa mataifa (ILO) limesema pamoja na Tanzania kuwa na mikakati mingi ya kutaka kuwakwamua wananchi wake na Lindi la umaskini itakuwa vigumu kufikiwa kwa lengo hilo kutokana na kuwa na watu wengi wa

Mwakilishi wa Shirika la Kazi Duniani nchini Tanzania (ILO) Bw. Alexio Musindo.

Akizungumza na wataalam na watafiti wa idara za kazi ajira na takwimu kutoka mikoa mbalimbali nchini mratibu wa sera na ajira wa shirika hilo hapa nchini Bi. Flora Minja amesema pamoja na Tanzania kuwa na tatizo kubwa la ukosefu wa ajira asilimia kubwa ya waliobahatika kuwa na ajira wanafanya kazi katika viwango vya chini ambavyo havikidhi mahitaji.

Mkurugenzi wa ajira kutoka wizara ya kazi Bw, Ally Msaki amesema tayari Wizara imeshaanza kushughulikia changamoto hiyo ikiwa ni pamoja na kuanza kufanya utafiti nchi nzima utakaosaidia kutoa takwimu za idadi ya watu wenye uwezo wa kufanya kazi na mchango wao katika uzalishaji.

Akizungumzia tatizo hilo mkurugenzi wa ofisi ya sensa na takwimu nchini Ephrahim Kwesigabo amesema ofisi ya takwimu kwa kushirikiana na shirika la kazi duniani inaendelea kuwajengea uwezo watafiti na wataalam nchini ili waweze kuisaidia serikali kubainisha ukubwa wa tatizo na kuishauri kupata ufumbuzi.

Akifungua mafunzo kwa wataalam na watafiti hao katibu tawala wa mkoa wa Arusha bw. Addo Mapunda amesema kukosekana kwa tija katika uzalishaji kunachangiwa na dhana iliyojengeka hasa kwa vijana ya kuajiriwa badala ya kujiajiri na kufanya kazi kwa mazoea tatizo ambalo ufumbuzi wake unahitaji ushirikiano wa wadau wengi.