Sunday , 27th Apr , 2014

Idadi ya watoto wanaozaliwa na ugonjwa wa kisukari nchini Tanzania imeongezeka kutoka asilimia 15 hadi asilimia 28.

Daktari bingwa wa watoto wanaougua kisukari Dkt Edna Majaliwa ametaja sababu ya ongezeko hilo kuwa ni kutokana na kiwango kidogo cha protini ambacho akina mama wajawazito wanakuwa nacho wakati wa ujauzito wao.

Kwa mujibu wa Dkt Majaliwa, ukosefu wa protini kwa akina mama wajawazito kunasababisha upungufu wa kemikali aina ya insulini katika miili ya watoto wanaozaliwa, kemikali ambayo hutumika kurekebisha kiwango cha sukari katika mwili wa binadamu.