Wednesday , 23rd Apr , 2014

Mwenyekiti wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi Tanzania (Tucta) mkoa wa Mbeya, Alinanuswe Mwakapala, amesema idadi kubwa ya wafanyakazi wanalipwa mishahara chini ya kiwango na hawajajiunga na chama chochote cha wafanyakazi.

Waziri wa kazi na ajira Bi. Gaudensia Kabaka (kulia) akifafanua jambo

Mwakapala amesema wafanyakazi wengi wanalipwa chini ya kiwango kilichoainishwa na serikali, na hiyo inatokana na wafanyakai hao kutojiunga na vyama vya wafanyakazi ambavyo vingewatetea.

Amesema kwa sasa vyama vya wafanyakazi vipo katika mchakato wa kuandikisha wafanyakazi katika taasisi mbalimbali na kuwaelimisha wafanyakazi hao ili wazijue haki zao.