Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), Fatou Bensouda,
Akitangaza uamuzi huo, Bi Fatou Bensouda amesema kuwa amekuwa akifuatilia hali nchini, Burundi tangu mwezi Aprili 2015, akitoa wito wa mara kwa mara kwa pande zote zijiepushe na ukatili, na kuonya kuwa wanaotenda uhalifu unaotambuliwa chini ya mamlaka ya ICC watawajibishwa Kama watu binafsi.
Amesema tathmini ya awali siyo uchunguzi, lakini ni mchakato wa kufanyia tathmini taarifa zilizopo ili kuamua iwapo vigezo vya kuanza kufanya uchunguzi vimetimizwa, kulingana na Mkataba wa Roma.
Katika mzozo unaoendelea nchini Burundi, zaidi ya watu 430 wameripotiwa kuuawa, huku watu wapatao 3,400 wakiwa wamekamatwa, na zaidi ya 230,000 kulazimika kuhama makwao.