Monday , 21st Mar , 2016

Hospitali ya Sokoine Mkoani Lindi inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja na upungufu wa wahudumu na Madaktari hali inayosababisha hospitali hiyo kubwa ya serikali ishindwe kutoa huduma inavyostahili.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Godfrey Zambi.

Hayo yamebainika katika ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi alipotembelea hospitali hiyo kujionea huduma zinavyotolewa na pia kuwajulia hali wagonjwa wanaopata matibabu hospitalini hapo.

Mkuu huyo wa Mkoa amewataka watumishi wa Hospitali hiyo licha ya kutaka kulipwa madai yao lakini wanapaswa kutoa huduma kwa kuzingatia weledi pamoja na utu kwa wagonjwa hasa kwa kina mama wajawazito.

Akizungumza na viongozi wa Hospitali hiyo akiwemo Mganga wa Mkoa, Kaimu Mganga mfawidhi wa Hospitali na katibu wa Hospitali na kusema kuwa ameridhika na utoaji wa matibabu katika hospitali hiyo licha ya changamoto hizo wanazokabiliana nazo.