Friday , 5th Feb , 2016

Licha ya serikali ya India kutangaza kuwa watu 5 wamekamatwa kwa kosa la kuwashambulia na kumvua nguo mwanafunzi mmoja raia wa Tanzania, hofu bado imetanda miongoni mwa takriban wanafunzi 150 wa chuo cha Acharya Kaskazini mwa Bangalore .

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kanda na Kimataifa, Balozi Augustine Mahiga

Wawakilishi wa wanafunzi hao wameiambia BBC kuwa uoga na hofu ya kutokea kwa mashambulizi zaidi dhidi yao ndio imewafanya watanzania hao kukataa kutoka makwao wakihofia usalama wao.

Hata mkutano ulioitishwa na bodi inayosimamia chuo hicho cha Acharya haukuhudhuriwa na wanafunzi kutokana na tishio la usalama wao.

Shambulizi hilo liliwakumba wanafunzi wa kike raia wa Tanzania ambao bila ya kujua kilichokuwa kimejiri walipita karibu na eneo ambalo mwanafunzi mmoja raia wa Sudan Kusini alikuwa amemgonga na kumuua mwanamke mmoja mhindi

Hata hivyo jana tayari serikali ya Tanzania imesema kuwa imeshapeleka dokezi la kidiplomasia kwa serikali ya India ili kuonesha kukasirishwa na kitendo hicho ikiwa ni pamoja na kuwahakikishia usalama wanafunzi hao raia wa Tanzania.

CHANZO BBC