
Rais Dkt. John Magufuli.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Jumapili Novemba 4, 2018 wakati akitoa salamu zake kwenye maadhimisho ya miaka 150 ya Ukatoliki Tanzania Bara yaliyofanyika Bagamoyo mkoani Pwani, ambapo amesema licha ya changamoto nyingi anazokutana nazo katika uongozi wake, haishi kujiuliza maswali viongozi waliopita walitumia mbinu gani kuhakikisha wanatatua yale waliyokumbana nayo.
“Nahitaji maombi sana kutoka kwenu na hata maoni, changamoto za kazi hizi ni ngumu sana nawaza hivi hawa wazee walionitangulia kina Mzee Kikwete, Mkapa na Mwinyi walimalizaje miaka 10, ni kazi nzito inahitaji maombi kwelikweli", amesema Magufuli.
Kwa Upande wake Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Nairobi nchini Kenya, John Kadinali Njue amesema hakuna mwanadamu aliyeumbwa kwa bahati mbaya huku akiwataka wanaadamu kutekeleza makusudi ya Mungu kwa kutenda mema.
"Vijana nanyi timizeni wajibu wenu, vaeni mavazi ya maadili muwe na amani na nyie watoto kueni kwa kutunza nidhamu, huu ni wakati wa kujiuliza mbegu ya imani iliyopangwa na wamishenari wetu wakati wa kuanza kanisa hili inatunzwa," amesema.