Tuesday , 21st Jul , 2015

Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambaye ni mbunge aliyemaliza muda wake katika jimbo la Mtwara vijijini, Mhe. Hawa Ghasia, amekuwa ni mgombea pekee wa ubunge alierudisha fomu kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM katika jimbo hilo.

Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambaye ni mbunge aliyemaliza muda wake katika jimbo la Mtwara vijijini, Mhe. Hawa Ghasia.

Akizungumza na East Africa Radio kwa njia ya simu, katibu wa CCM wilaya ya Mtwara vijijini, Amina Imbo, amesema wilaya yake ina majimbo mawili ambayo ni la Mtwara vijijini na Nanyamba, ambapo awali idadi ya waliojitokeza kuchukua fomu kwa majimbo yote ilikuwa ni wanne lakini waliorudisha ni watatu.

Awali jimbo hilo lilipata wagombea wawili wa CCM waliokuwa wamechukua fomu ambao ni Hawa Ghasia na Selemani Libubulu, lakini mpaka mwisho wa zoezi la kuchukua na kurudisha fomu ulipofika Julai 19 saa 10 alasiri, ni Ghasia pekee ambaye alifanikiwa kurudisha na kujikuta hana mpinzani kutoka chama chake katika nafasi hiyo.