
Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema
Kwa mujibu wa Godbless Lema ametoa maelezo kwa jeshi hilo ambapo amesema alishauri kuongeza nguvu juu ya namna ya kupambana na matukio ya kiuhalifu.
“Kwenye ule mkutano wangu na waandishi ilionekana kuna vitu nilizungumza ni muhimu, kwa hiyo nimelishauri jeshi la polisi kwamba sitaacha kulionya muda wowote ule kama Waziri Kivuli wa Wizara ya Mambo ya ndani.” amesema Lema.
“Wasione watu tunazungumza wakadhani kwamba tutatumiwa na mabeberu, hatutumiki Ila tunatafakari miaka 50 inayokuja jeshi la polisi litakuaje”, ameongeza Mbunge huyo.
Mapema jana Jumapili kupitia ukurasa wake wa twitter, Lema aliandika ujumbe kukiri kuitwa na jeshi la polisi jijini Arusha kwaajili ya kutoa maelezo.
Juzi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam IGP Simon Sirro alisema "niwaombe sana watu hawa wajitahidi kushirikiana na vyombo vya dola na kama wanatumika vibaya ili kuvikwamisha vyombo vya dola hatutawapa nafasi, na wananchi mnaona jana walianza kuzungumza kwenye mitandao lakini leo mmeona amepatikanana.”